Kitengo cha mahusiano kimeandaa ratiba ya kidini na kitamaduni kwa ugeni wa vijana kutoka nchi tofauti.

Kitengo cha mahusiano katika Atabatu Abbasiyya, kimeandaa ratiba ya kidini na kitamaduni kwa ugeni wa vijana kutoka nchi tofauti.

Kiongozi wa idara ya maelekezo ya kidini na muhadhiri Sayyid Muhammad Mussawi amesema “Tumepokea kundi la vijana kutoka nchi za magharibi na tumefanya kikao, wameongea zaidi kuhusu changamoto wanazopata kwenye nchi wanazo ishi”,

Akaongeza kuwa “Tumeongea mada tofauti zikiwemo za Fiqhi na Akhlaq, tukajikita zaidi katika mada ya Aqida”, akasema “Vijana wameuliza maswali mengi na yote wamejibiwa”.

Akaendelea kusema “Ziara hii imesimamiwa na watumishi wa kitengo cha mahusiano na wataendelea kuwasiliana nao sambamba na kufungua taasisi za kidini na kijamii, kwa ajili ya kufanya Tablighi katika nchi hizo”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: