Atabatu Abbasiyya tukufu imezindua makaburi ya Raudhat Jannatul-Kafeel ya wahanga waliouwawa na utawala wa chama cha Ba’ath katika mji wa Najafu.

Atabatu Abbasiyya imefungua makaburi ya Raudhat Jannatul-Kafeel ya watu waliouwawa na utawala wa chama cha Ba’ath katika mkoa wa Najafu Ashrafu.

Ufunguzi huo umefanywa katika hafla ya kumbukumbu katika makaburi ya mfano mkoani Najafu ya watu waliouwawa kwenye gereza la Badushi.

Ufunguzi huo umehudhuriwa na baadhi ya wajumbe wa kamati kuu ambao ni, Sayyid Liith Mussawi, Sayyid Jawadi Hasanawi na baadhi ya marais wa vitengo, muwakilishi wa Waziri mkuu Muheshimiwa Zidani Khalfu, Waziri wa uadilifu Muheshimiwa Khalidi Shawani na rais wa taasisi ya Mashahidi Muheshimiwa Abdul-Ilahi Naailiy.

Mkuu wa kituo cha kiiraq cha kuthibitisha jinai za magaidi chini ya kitengo cha Habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya Dokta Abbasi Quraishi amesema, “Hakika Atabatu Abbasiyya imefungua makaburi ya (Raudhat Jannatul-Kafeel) maalum kwa watu waliouwawa na utawala wa Ba’ath na makundi ya kigaidi, huu ni Ushahidi wa kihistoria kwa jinai zilizofanywa na Daesh kwa raia wa Iraq”.

Akaongeza kuwa “Makaburi haya wamezikwa kundi la kwanza la watu waliouwawa katika gereza la Badushi mwaka 2014m, baada ya magaidi wa Daesh kuteka gereza hilo na kuuwa watu hovyo kwa misingi ya umadhehebu na utabaka”.

Akaendelea kusema “Atabatu Abbasiyya imeshughulikia kazi zote za maziko na kuhakikisha marehemu hao wanalazwa katika nyumba zao za mwisho kwa kufuata taratibu zote za kisheria”.

Akamalizia kwa kusema “Leo tunakumbuka mauwaji ya wafungwa wa gereza la Badushi na tunatuma salamu kwa umoja wa mataifa kuhusu mauwaji haya ya kinyama”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: