Kituo cha utamaduni wa familia kimeratibu muhadhara kwa watumishi wa chuo kikuu cha Al-Ameed.

Kituo cha utamaduni wa familia katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kimeratibu muhadhara wenye anuani isemayo (Wewe ni nani?) kwa watumishi wa chuo kikuu cha Al-Ameed.

Mkuu wa Markazi bibi Sara Hafaar amesema “Muhadhara huo ni sehemu ya ratiba endelevu ya kituo katika vyuo vikuu, yenye anuani isemayo (Chemchem ya utamaduni katika korido za Al-Ameed), chini ya uhadhiri wa Dokta Shaimaa Nasoro mbobezi wa tiba (mambo) ya kisaikolojia na kimaadili”.

Akaongeza kuwa “Muhadhara unalenga kujenga uwezo wa watumishi wa kitengo cha ushauri nasaha katika chuo cha Al-Ameed”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: