Kitengo kinacho simamia uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu kinasafishia mitende iliyopo katika eneo hilo takatifu.

Kitengo kinachosimamia uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu katika Atabatu Abbasiyya, kinasafishia mitende iliyopo kwenye eneo hiyo takatifu.

Kiongozi wa idara ya miti chini ya kitengo hicho Sayyid Haatim Abdulkarim amesema “Watumishi wa idara yetu wameanza kazi ya kusafishia mitende iliyopo katika eneo la katikati ya haram mbili takatifu”.

Akaongeza kuwa “Kazi hiyo inahusisha kuchambulia majani ya mitende na kusafisha sehemu ya shina, na kuifanya kuwa na muonekano mzuri unaoendana na eneo hili tukufu, sambamba na kuindaa kwa ajili ya msimu wa kupamba”.

Watumishi wa kitengo kinachohudumia uwanja wa katikati ya haram mbili, wanaratiba maalum ya msimu wa masika ikiwa ni Pamoja na kupangilia vizuri bustani zake na kuchambulia aina zote za miti kwa ajili ya kuweka muonekano mzuri wa eneo hilo mbele ya mazuwaru wa Ataba mbili takatifu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: