Kiongozi wa idara bibi Fatuma Abbasi Mussawi amesema “Idara imeanza mitihani ya nusu mwaka kwa wanafunzi (100), baada ya kumaliza muhula wa masomo”.
Akaongeza kuwa “Maswali yameandaliwa na kamati maalum katika somo la Fiqhi, Aqida, Nahau, Hukumu za usomaji, Balagha, Uluumul-Qur’ani, maswali yote yameandaliwa vizuri kutokana na selebasi ya masomo”.
Akaendelea kusema “Kabla ya kuanza mitihani tulifanya kikao, kwa ajili ya kuchagua kamati itakayo husika na kuhakiki maswali pamoja na kuandaa daftari za mitihani kwa kufuata misingi ya kielimu”.