Atabatu Abbasiyya imeandaa ratiba ya kitamaduni kwa ugeni wa wanafunzi kutoka Baabil.

Atabatu Abbasiyya tukufu imeandaa ratiba ya kitamaduni kwa ugeni wa wanafunzi kutoka shule ya Imamu Hussein (a.s) katika mkoa wa Baabil.

Muhadhiri Sayyid Hassan Ali Jawaadi amesema “Atabatu Abbasiyya tukufu imeandaa ratiba tofauti, zinazohusu watu wa tabaka tofauti likiwemo tabaka la wanafunzi, kwa lengo la kulinda utamaduni na utambulisho wao kutokana na hatari za kifikra na athari za mitandao ya kijamii”.

Akaongeza kuwa “Ratiba imepambwa na nadwa, umetolewa muhadhara kuhusu Akhlaq, kuheshimu wazazi, walimu kujipamba na maadili mema, mambo ambayo ni muhimu katika utafutaji wa elimu”.

Msimamizi wa ratiba hiyo Sayyid Halo amesema “Muhadhara umejikita katika Akhlaq na kutengeneza jamii yenye mafungamano na Ahlulbait (a.s) na imesisitizwa sana sekta ya elimu”.

Wanafunzi wameshukuru Atabatu Abbasiyya tukufu kwa kazi kubwa inayofanya ya kuhudumia wanafunzi na jamii kwa ujumla.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: