Hivi karibuni kitengo cha Habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya, kupitia kituo cha tafiti za kiislamu na kimkakati, kimechapisha juzuu la 13 la kitabu cha (Uovu wa tamaduni za kimagharibi).
Juzuu jipya limepewa anuani isemayo “Uovu wa tamaduni za kimagharibi” linamambo makuu matatu (Historia – Siasa – Jamii), Ulaya katika zama za kati, kuanzishwa kwa mfumo wa elimu ya kimagharibi, juzuu hili limeandikwa na kundi la watafiti.
Mfululizo wa kitabu hiki unalenga kuonyesha historia ya nchi za Magharibi kwenye kila nyanja. Elimu, Dini, Utamaduni, Jamii, Siasa, Uchumi, mambo hayo tunayaangazia kwenye kila muongo (zama), kuanzia miaka ya kale hadi zama hizi, tambua kuwa historia ya nchi za Ulaya inafika hadi miaka elfu nne, imejaa mambo ya hovyo yasiyokubalika na mtu mwenye akili.