Msomaji wa Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya Haafidh (Hussein Alghazi) amekuwa mshindi wa kwanza kwenye shindano la kitaifa la kuhifandi Qur’ani awamu ya kumi na nne, lililofanyika jijini Baghdad.
Shindano hilo limesimamiwa na kituo cha kitaifa cha masomo ya Qur’ani chini ya Atabatu Alkadhimiyya tukufu, lilikuwa na kauli mbiu isemayo (Iraq ni Fahari kwa wote) washiriki walikuwa mahaafidh (60) kutoka mikoa tofauti ya Iraq chini ya kamati ya majachi mahiri.
Tambua kuwa Haafidh Hussein Alghazi ni mmoja wa walimu wa Maahadi ya Qur’ani na msomaji wa tawi la Baghdad chini ya Majmaa, amefanikiwa kuingia kwenye mashindano ya kimataifa baada ya kuibuka mshindi wa kwanza kwenye shindano hili.