Kitengo cha kusimamia haram tukufu katika Atabatu Abbasiyya, kimeweka mazingira ya furaha na shada za mauwa ndani ya ukumbi wa malalo ya Abulfadhil Abbasi kufuatia kumbukumbu ya kuzaliwa Bibi Fatuma Zaharaa (a.s).
Makamo rais wa kitengo hicho Sayyid Zainul-Aabidina Quraishi amesema “Watumishi wa kitengo chetu wameweka mazingira ya furaha ndani ya Ataba tukufu, kufuatia kumbukumbu ya kuzaliwa mbora wa wanawake wa ulimwenguni (a.s)”.
Akaongeza kuwa “Tumeweka mauwa ndani ya Ataba tukufu na kwenye Barabara zinazoelekea Ataba, yakiwa ni maandalizi ya kufanya hafla katika eneo la mlango wa Kibla ya Abulfadhil Abbasi (a.s), aidha tumeandaa pipi, mauwa na zawadi”.
Akaendelea kusema “Kamati ya makongamano na hafla imeanza kuandaa majukwaa katika eneo la ukanda wa kijani kibichi, vitalu vya Alkafeel na maeneo mengine yaliyochini ya Atabatu Abbasiyya tukufu”.