Kitengo cha uboreshaji na maendeleo endelevu katika Atabatu Abbasiyya, kinafanya semina ya (Diplomasia ya mahusiano) kwa watumishi wa idara ya mawasiliano.
Sayyid Ali Hasun Shimri amesema “Semina inalenga kuwajengea uwezo watumishi wetu kwenye sekta ya mahusiano na kukuza vipaji vyao katika mahusiano na watu wanaoamiliana nao na kujenga mahusiano mapya pamoja na viongozi na wafanyakazi wenzao”.
Akaongeza kuwa “Wanasemina wamefundishwa misingi ya kazi sambamba na mbinu za mawasiliano katika kutekeleza majukumu yao”.
Semina inafanywa ndani ya ukumbi wa Naafidhu-Albaswirah, itadumu kwa muda wa siku nne, kila siku wanasoma kwa muda wa saa tatu.