Atabatu Abbasiyya imeanza shindano maalum kuhusu mazazi ya Bibi Zaharaa (a.s).

Uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu umetangaza shindano la kitamaduni linalohusu kuzaliwa kwa Bibi Fatuma Zaharaa (a.s).

Majina ya washindi kumi yatatangazwa jioni ya Jumatatu sawa na tarehe (1/1/2024) saa moja jioni kwenye jukwaa la Ataba tukufu.

Sharti la kupokea zawadi mshindi anatakiwa kuwepo kwenye hafla ya mazazi ya Bibi Fatuma Zaharaa (a.s), itakayo fanywa katika eneo la mlango wa Kibla ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) siku ya Jumanne (2/1/2024m) sawa na mwezi (19 Jamadal-Aakhar 1445h).

Iwapo mshindi atashindwa kuhudhuria, atatakiwa afike kwenye kitengo cha mali ndani ya siku zisizozidi (4) toka kutangazwa kwa matokeo hayo, akiwa na vielelezo vya kumthibitisha (kitambulisho cha uraia au hati ya kusafiria).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: