Ugeni kutoka idara ya kilimo ya Baabil umepongeza miradi ya kilimo inayofanywa na Atabatu Abbasiyya.

Ugeni kutoka idara ya kilimo ya mkoa wa Baabil umepongeza miradi ya kilimo inayofanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu.

Dokta Haidari Falahu mmoja wa wageni hao amesema “Tumefanya ziara hii kwa ajili ya kutambua miradi ya kilimo inayofanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu, likiwemo shamba la Saaqi”. Akabainisha kuwa “Ugeni huu umejumuisha wasomi wenye shahada za juu katika mambo ya kilimo”.

Akaongeza kuwa “Shamba la Saaqi linamchango mkubwa katika sekta ya kilimo hapa nchini, kwani shamba hili linatende za aina tofati na aina zingine za vyakula kama Zaituni”.

Akaendelea kusema “Atabatu Abbasiyya inatilia umuhimu mkubwa kilimo kwa kuwa ndio nguzo ya msingi katika kuhakikisha upatikanaji wa chakula”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: