Wizara ya kilimo imesema: Miradi ya kilimo inayofanywa na Atabatu Abbasiyya ni muhimu kwa sekta ya kilimo.

Wizara ya kilimo imesema kuwa miradi ya Atabatu Abbasiyya ni mizuri na inasaidia sana sekta ya kilimo hapa nchini.

Yamesemwa hayo wakati wa ziara iliyofanywa na idara ya mipango kutoka wizara ya kilimo kwenye baadhi ya miradi ya Atabatu Abbasiyya tukufu.

Makamo rais wa wahandisi wa kilimo katika wizara Sayyid Ali Ghaalib Saidi amesema “Ziara imehusisha kutembelea baadhi ya miradi ya kilimo inayofanywa na Atabatu Abbasiyya, ukiwemo mradi wa shamba la Awali na Firdausi, tumebaini kuwa miradi hiyo inamchango mkubwa katika sekta ya kilimo hapa nchini, aidha inasaitia upatikanaji wa chakula kwa raia tena kwa bei nafuu”.

Mkuu wa idara ya kilimo wa mkoa wa Karbala Muhamdisi Muhammad Jaasim Twayari amesema “Atabatu Abbasiyya inaendesha miradi muhimu katika jangwa la Karbala, ukiwemo mradi wa shamba la Firdausi, unaohusika na kilimo cha viazi mviringo, mwaka huu wamelima karibu Dunam elfu moja”.

Akaongeza kuwa “Wageni wameambiwa mkakati wa pili wa mradi huo, uliopangwa kwa kushirikiana na idara ya kilimo ya mkoa wa Karbala”, akasema “Wageni wamepongeza kilimo cha kisasa kinachofanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: