Mtafiti kutoka Lebanon Zahara Malidan amesema kuwa, Kongamano la Ruhu Nubuwwah linalosimamiwa na Atabatu Abbasiyya tukufu, ni tunda litakalochumwa na watoto wetu.
Ameyasema hayo pembezoni mwa kongamano linaloendeshwa na idara ya shule za Dini Alkafeel katika Atabatu Abbasiyya tukufu, chini ya kauli mbiu isemayo (Fatuma Zaharaa amekusanya nuru mbili ya Utume na Uimamu), ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha mazazi ya Swidiqatu Kubra Fatuma Zaharaa (a.s).
Akasema kuwa “Hakika kongamano hili ni tunda litakalochumwa na watoto wetu katika kuhuisha historia ya Bibi Fatuma Zaharaa (a.s) na kuwa mtazamo wa Abulfadhil Abbasi (a.s) aliyekuwa mtu mwenye mtazamo na ushujaa”.
Akaongeza kuwa “Amepongeza mafanikio ya kongamano hili katika zama zenye changamoto nyingi”.
Amesifu Atabatu Abbasiyya kwa kusema “Naipomgeza Atabatu Abbasiyya tukufu kwa mafanikio makubwa tuliyo shuhudia, amma kwa hakika furaha yetu ni kubwa mmno haielezeki”.