Msomaji wa Qur’ani tukufu Bibi Hauraa Hamza kutoka Lebanon amesema kuwa, Kongamano la Ruhu-Nubuwah linaonyesha picha mpya ya mwanamke wa kiislamu katika zama zetu.
Ameyasema hayo pembezoni mwa kongamano linalosimamiwa na idara ya shule za Dini Alkafee katika Atabatu Abbasiyya, chini ya kauli mbiu isemayo (Fatuma Zaharaa amekusanya nuru mbili ya Utume na Uimamu), ambalo ni sehemu ya kuadhimisha mazazi matakatifu ya Bibi Fatuma Zaharaa (a.s).
Akasema “Yanayo shuhudiwa kwenye kongamano hili yanaonyesha uhalisia wa Iraq, hakika Bibi Zaharaa (a.s) ni chemchem ya elimu na kumzungumzia kunajenga picha mpya ya mwanamke wa zama zetu, na kuonyesha namna gani anaweza kufikisha ujumbe kwa jamii katika taifa lolote atakapokua”.
Akaongeza kuwa “Nimejikuta kuwa naweza kufikisha sauti yangu kwa kusoma Qur’ani tukufu na kushiriki pamoja na wengine, hakika hii ni fursa nzuri sana kuwepo hapa katika ardhi tukufu, natamani ijurudie tena katika awamu zijazo”.
Akaendelea kusema “Shukrani za pekee ziiendee Atabatu Abbasiyya tukufu kwa kunipa nafasi ya kuja kushiriki kwenye kongamano hili, na kuzungumzia swala hili muhimu, hususan tukio hili takatifu”.