Kitengo cha habari na utamaduni kimeadhimisha mazazi ya Bibi Zaharaa (a.s) nchini Tanzania.

Kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya, kimeadhimisha mazazi ya mbora wa wanawake wa ulimwenguni Fatuma Zaharaa (a.s) katika mkoa wa Pwani nchini Tanzania.

Mkuu wa Markazi Dirasaati Afriqiyya Shekhe Saadi Shimri amesema, kuadhimisha matukio yanayohusu Ahlulbait katika bara la Afrika ni moja ya malengo ya Markazi, jambo hilo linamchango mkubwa wa kufikisha mafundisho ya Ahlulbait (a.s) kwa tabaka zote za waafrika, pia jambo hilo ni kuhuisha alama za Dini”.

Akaongeza kuwa “Markazi imefanya hafla ya kuadhimisha mazazi ya Fatuma Zaharaa (a.s) katika mkoa wa Pwani nchini Tanzania, wameshiriki wafuasi na wapenzi wa Ahlulbait (a.s) chini ya usimamizi wa muwakilishi wa Markazi Shekhe Kiza Mussa”.

Akaendelea kusema “Hafla imehusisha utoaji wa muhadhara na usomaji wa qaswida na mashairi kuhusu utukufu wa Bibi Zaharaa (a.s), sambamba na ujumbe wa Markazi uliotolewa na shekhe Kiza Mussa, amefafanua nafasi ya Fatuma Zaharaa (a.s) na historia yake, sambamba na kufafanua sifa za mwanamke bora”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: