Majmaa-Ilmi imeadhimisha mazazi ya Bibi Fatuma Zaharaa (a.s) katika chuo kikuu cha Karbalaa.

Majmaa-Ilmi ya Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya tukufu imeadhimisha mazazi ya Swidiqatu Kubra Fatuma Zaharaa (a.s) kwa kufanya majlisi ya usomaji wa Qur’ani katika chuo kikuu cha Karbala.

Majlisi hiyo ni sehemu ya mradi wa hafla za usomaji wa Qur’ani katika vyuo vikuu vya Iraq, unaosimamiwa na kituo cha miradi ya Qur’ani chini ya Majmaa, kwa kushirikiana na kitivo cha Tarbiyya katika chuo kikuu cha Karbala.

Majlisi imefanywa ndani ya kumumbi mkuu wa chuo na kuhudhuriwa na rais wa Majmaa-Ilmi Dokta Mushtaqu Ali, rais wa chuo kikuu cha Karbala Dokta Basim Khalili Naail na wasaidizi wake, aidha alikuwepo pia rais wa Jaamia ya Bibi Maasumah kutoka Iran Dokta Maryam Barbara, walimu wa chuo, wasomi wa kisekula, viongozi wa idara na wanafunzi wakiume na wakike.

Majlisi imefunguliwa kwa Qur’ani tukufu iliyosimwa na Hasanaini Jazaairi na Haidari Muhsin Albazuni, ukafuata muhadhara kutoka kwa Shekhe Zamani Hasanawi, ameongea kuhusu umuhimu wa kulinda misingi ya uislamu na utaifa sambamba na misingi ya maadili mema ambayo ndio njia ya kufaulu kwa mwanadamu hapa duniani, aidha amewahimiza wanafunzi kujituma katika kutafuta elimu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: