Kongamano linasimamiwa na idara ya shule za Alkafeel za wasichana katika Atabatu Abbasiyya chini ya kauli mbiu isemayo (Fatuma Zaharaa amekusanya nuru mbili ya Utume na Uimamu) katika kuadhimisha mazazi ya Swidiqatu-Kubra Fatuma Zaharaa (a.s) iliyokuwa na vipengele tofauti.
Siku ya tatu imekuwa na vikao viwili, cha asubuhi na jioni, kwenye kila kika kulikuwa na uwasilishaji wa mada nne za kielimu, kikao cha asubuhi kimesimamiwa na makamo rais wa chuo kikuu cha Alkafeel Dokta Nawaal Aaidi Almayali na muendesha kikao alikuwa Dokta Imani Swalehe Mahadi kutoka kituo cha kuhuisha turathi za kielimu na kiarabu, kikao cha jioni kikaongonzwa na Dokta Karimah Muhammad Madani na muendeshaji wa kikao akawa Dokta Zaharaa Raufu Mussawi.
Siku mbili zilizopita kongamano limeshuhudia harakati tofauti, miongoni mwa harakati hizo ni kuonyeshwa filamu ya namna walivyo jitolea mashahidi watukufu, kukabidhi zawadi kwa familia za mashahidi, kufanya vikao vya kielimu, usomaji wa Qur’ani na mashairi, jumla ya nchi (14) za kiarabu na kiajemi zimeshiriki kwenye kongamano hili, ambazo ni: Kuwait, Saudia, Baharain, Oman, Lebanon, Misri, Tunisia, Moroko, Iran, Ufaransa, Uingereza, Italia, Hispania na Ubelgiji.