Mjumbe wa kamati kuu ya Atabatu Abbasiyya tukufu Dokta Abbasi Didah Mussawi amesema kuwa, kuna kamati itaudwa kwa ajili ya kufatilia maazimio ya kongamano la Ruhu-Nubuwah la kimataifa awamu ya sita na kuyafanyia kazi.
Kongamano linasimamiwa na idara ya shule za Alkafeel katika Atabatu Abbasiyya, chini ya kauli mbiu isemayo (Fatuma Zaharaa amekusanya nuru mbili ya Utume na Uimamu) sambamba na maadhimisho ya kuzaliwa kwa Swidiqatul-Kubra Fatuma Zaharaa (a.s).
Akasema kuwa “Ubora wa kazi huangaliwa mwisho wake, tupo mwishoni mwa kongamano la Ruhu-Nubuwah awamu ya sita, leo tumeona matunda ya kongamano hili kupitia mijadala, maswali na maoni ya washiriki ambayo yamepelekea kupatikana maazimio yatakayosomwa katika tamko la mwisho”.
Akaongeza kuwa “Itaundwa kamati maalum ya kufuatilia maazimio na kuyafanyia kazi”, akasema “Maazimio ni mazuri sana kwani yametokana na kongamano tukufu lililoangazia nuru ya Bibi Fatuma Zaharaa (a.s)”.