Miongoni mwa ratiba ya siku ya nne ya kongamano la Ruhu-Nubuwah la kimataifa awamu ya sita ni kikao chenye anuani isemayo (Swidiqah na Qur’ani).
Kongamano linasimamiwa na idara ya shule za Alkafeel za wasichana katika Atabatu Abbasiyya chini ya kauli mbiu isemayo (Fatuma Zaharaa amekusanya nuru mbili ya Utume na Uimamu), kongamano hili linafanywa sambamba na maadhimisho ya kuzaliwa kwa Swidiqatul-Kubra Fatuma Zaharaa (a.s).
Ratiba ya jioni imetekelezwa katika kituo cha Swidiqatu-Twahirah (a.s) chini ya Ataba tukufu, imefunguliwa kwa Qur’ani tukufu iliyosomwa na Hauraa Aamir Yasini, kisha muhadhiri kutoka Saudia akawasilisha mada isemayo (Swidiqah na Qur’ani).
Ameeleza nafasi ya Fatuma Zaharaa (a.s) na maana ya Alkauthar pamoja na uhusiano wake na Qur’ani tukufu, sambamba na kuangazia mambo yaliyomtokea (a.s).
Akafafanua namna Bibi Fatuma Zaharaa (a.s) alivyo pambana kulinda Qur’ani tukufu, akaeleza mazingira ya kifo chake na namna nzuri ya kuwanusuru mashahidi sio kwa kuuwa aliye muuwa tu, bali ni kufuata mwenendo wao na kuhuisha fikra zao kwa kufanya yale waliyotaka kuyafanya.
Kwa mujibu wa mtafiti kutoka Saudia “Upambanaji wa Fatuma Zaharaa (a.s) katika kulinda Qur’ani tukufu, kunaweka msingi wa kufantwa na kila mtu hadi Maasumina (a.s)”.