Kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya, kimeandaa ratiba ya masomo kwa ugeni wa vijana kutoka mkoa wa Dhiqaar.
Mkuu wa kituo cha kitamaduni Multaqal-Qamaru Shekhe Harithu Dahi amesema “Tawi la kituo katika mkoa wa Dhiqaar limeandaa ratiba maalum ya masomo kwa vijana walioteuliwa kwa kufuata vigezo na masharti yaliyowekwa”.
Akaongeza kuwa “Ratiba inavipengele vingi, warsha, mihadhara kuhusu mambo tofauti, mbinu za uwasilishaji, namna ya kuamiliana na kundi kubwa la watu na mambo mengine”.
Akaendelea kusema “Ratiba imedumu kwa wiki kadhaa, nayo ni moja ya ratiba muhimu inayafanywa na kituo cha Multaqal-Qamaru, kwa lengo la kuwajengea uwezo vijana kutoka mikoa yote”.