Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya, inaendelea na semina za Qur’ani kwa wakuu wa taasisi za Qur’ani, kupitia mradi wa kitaifa wa kuendeleza usomaji wa Qur’ani hapa Iraq.
Semina imeratibiwa na Maahadi ya Qur’ani tukufu katika mji wa Najafu chini ya Majmaa.
Kipindi cha jioni ya siku ya tatu ya semina kilifanyika kikao-kazi chenye anuani isemayo (Mipango mkakati ya kitaasisi), muwezeshaji alikuwa ni Ustadh Saadi Khalidi, amefafanua mipango mkakati ya ndani na nje ya taasisi, na mchango wa kila kimoja katika kuendeleza taasisi.
Akasisitiza umuhimu wa kila taasisi iwe na mpango mkakati wake, utakaosaidia kufikia malengo ya kuanzishwa kwake, sambamba na malengo yanayojitokewa wakati wa utendaji.
Semina itadumu kwa muda wa siku nne, inawashiriki (35) ambao ni wakuu wa taasisi za Qur’ani kutoka mikoa tisa, inapambwa na vikao vya majadiliano mbalimbali kwa lengo la kuboresha shughuli za Qur’ani hapa Iraq.