Kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya, kimeadhimisha mazazi ya mbora wa wanawake wa ulimwenguni Fatuma Zaharaa (a.s) katika nchi ya Seralion.
Mkuu wa Markazi Dirasaati Afriqiyya Shekhe Saadi Shimri amesema “Moja ya malengo ya Markazi ni kuhuisha matukio yanayowahusu Ahlulbait (a.s) katika bara la Afrika, jambo hilo linasaidia kwa kiwango kikubwa kufikisha mafundisho ya Dini katika jamii za waafrika sambamba na kuhuisha matukufu ya Dini”.
Akaongeza kuwa “Markazi imefanya hafla ya kuadhimisha mazazi ya Fatuma Zaharaa (a.s) katika mji wa Dafli nchini Seralion iliyokuwa na vipengele tofauti”.
Akasema: “Kulikuwa na muhadhara kuhusu historia ya Bibi Zaharaa (a.s) na umuhimu wa wanawake wa zama zetu kuiga mwenendo wake (a.s) pamoja na kubainisha mazingira aliyoishi na sifa za hijabu yake inayopaswa kuigwa, hafla imehudhuriwa na kundi la wafuasi na wapenzi wa Ahlulbait (a.s)”.