Kitengo cha malezi na elimu kimeshiriki kwenye matembezi ya kuadhimisha kuanzishwa kwa jeshi la Iraq.

Kitengo cha malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya, kupitia shule za Al-Ameed, kimeshiriki kwenye matembezi ya kuadhimisha miaka (103) tangu kuanzishwa kwa jeshi la Iraq.

Ushiriki huu ni kielelezo cha uzalendo wa taifa na kujenga misingi ya uzalengo katika nyoyo za wanafunzi na taasisi za kiraia.

Shule zilizo shiriki kwenye matembezi hayo ni, sekondari ya Sayyid-Almaau ya wavulana, Nurul-Ameed, Saaqi, Shule ya msingi Al-Ameed na shule zingine za hapa mkoani Karbala.

Walimu walioshiriki kwenye matembezi hayo, wameyasifu na kusema kuwa yanaimarisha uzalendo wa taifa na kujenga moyo wa kutumikia taifa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: