Uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya umetangaza shindano la kitamaduni kuhusu mazazi ya Imamu Muhammad Albaaqir na Ali Alhaadi (a.s).
Majina ya washindi yatatangazwa jioni ya Ijumaa (12/01/2024m) saa moja jioni, juu ya jukwaa la Atabatu Abbasiyya tukufu.
Sharti la kupokea zawadi, mshindi anatakiwa awepo kwenye hafla ya mazazi ya Imamu Muhammad Albaaqir na Ali Alhaadi (a.s), itakayofanywa katika eneo la mlango wa Kibla ya Abulfadhil Abbasi (a.s) siku ya Jumamosi (13/01/2024m) sawa na (1 Rajabu 1445h) saa nane jioni.
Uongozi wa Atabatu Abbasiyya umesema kuwa, iwapo mshindi atakuwa na udhuru wa kuhudhuria kwenye hafla hiyo, atatakiwa kufika kwenye ofisi za mali (wahasibu) katika Atabatu Abbasiyya ndani ya siku nne (4) akiwa na nyaraka zinazomthibitisha (kitambulisho cha taifa au hati ya kusafiria).