Kukamilika kwa maandalizi ya ufunguzi wa uwanja wa Abulfadhil Abbasi (a.s).

Watumishi wa kitengo cha ukanda wa kijani chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, wamekamilisha maandalizi ya ufunguzi wa uwanja wa Abulfadhil Abbasi (a.s).

Rais wa kitengo Sayyid Nasoro Hussein Mut’ibu amesema “Watumishi wa kitengo chetu wamekamilisha maandalizi ya ufunguzi wa uwanja wa Abulfadhil Abbasi (a.s), utakao ingizwa kwenye orodha ya viwanja vya ukanda wa kijani vipatavyo 24”.

Akaongeza kuwa “Maandalizi yamehusisha kutengeneza sehemu maalum za kukaa familia ndani ya eneo hilo, umetengenezwa mmiminiko wa maji mkubwa uliopambwa kwa miti na mauwa, sehemu hiyo ni nzuri kwa mapumziko ya familia za ndani na nje ya mji wa Karbala”.

Akafafanua kuwa “Miongoni kwa kazi zilizofanywa ni upandaji wa miti na mauwa kwa lengo la kupendezesha eneo hilo”, akasema kuwa “Atabatu Abbasiyya inaendelea na upandaji wa zaidi ya mitende na miti laki mbili (200,000) katika maeneo ya ukanda wa kijani”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: