Kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya, kimeadhimisha kifo cha mbora wa wanawake wa ulimwenguni Fatuma Zaharaa (a.s) katika mji wa Barako nchini Benin.
Mkuu wa Marka Dirasaati Afriqiyya Shekhe Saadi Shimri amesema “Markazi inafanya kila iwezalo katika kuendesha program zinazounganisha waislamu na kuondoa chuki na mfarakano katika nchi za Afrika, sambamba na kujenga mapenzi na mshikamano baina yao”.
Akaongeza kuwa “Mubalighi wa Markazi na muwakilishi wetu katika nchi ya Benin Shekhe Hassan Amidu, ameandaa hafla iliyohudhuriwa na viongozi kadhaa wa mji wa Barako, akahimiza umuhimu wa umoja wa waislamu na kuacha malumbano na mifarakano”.
Akaendelea kuwa “Hafla imepambwa na muhadhara kuhusu historia ya Bibi Zaharaa (a.s) na umuhimu wa wanawake wa zama hizi kufuata mwenendo wake (a.s)”.