Kitengo cha Dini kimetoa mihadhara ya kiitikadi na kifiqhi kwa watumishi wapya.

Kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kimetoa mihadhara ya kiitikadi na kifiqhi kupitia ratiba ya kuandaa watumishi wapya wa Ataba tukufu.

Mkufunzi wa semina Shekhe Fataahu Thaamir Baraghushi amesema
“Mihadhara ya Aqida, Fiqhi na Akhlaq imetolewa kwa watumishi wapya wa Atabatu Abbasiyya kupitia ratiba maalum”.

Akaongeza kuwa “Mihadhara imehusisha kujadili changamoto, hususan baadhi ya mambo ya kifiqhi yanayo husiana na swala, udhu na kuoga, kwa lengo la kulinda fikra za watumishi kutokana na baadhi ya mambo yanayohusu itikadi zao”, akasema kuwa “Mihadhara imepata muitikio mkubwa kutoka kwa washiriki”.

Akasema “Mihadhara ilikuwa na upekee wa kuongelea mambo ya kidini na kitamaduni, hakika imeongeza uwelewa wa washiriki katika mambo ya Dini na Akhlaq”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: