Sayyid Swafi amesema: Uwepo wa Sayyid Sistani nchini Iraq unawapa wananchi utulivu na maneno yake hutibu majeraha.

Kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Sayyid Ahmadi Swafi amesema kuwa, uwepo wa Marjaa Dini mkuu Sayyid Ali Sistani kunawapa utulivu wananchi na maneno yake hutibu majeraha.

Ameyasema hayo wakati akipokea ugeni wa taasisi ya Ahlulbait (a.s) kutoka Hispania.

Amesema kuwa “Sayyid Sistani ni Marjaa-Dini mkubwa, anaheshima kubwa hapa nchini na duniani kote, pamoja na kuwa ni Marjaa-Dini mkubwa, anahekima sana, anaishi na raia wa Iraq wa tabaka zote kama baba, amekuwa kimbilio la wote bila ubaguzi”, akabainisha kuwa “Wakati wa vitendo vya ugaidi vilivyo ikumba Iraq tangu mwaka wa (2003) amesimama kama baba wa raia wote wa Iraq”.

Akaongeza kuwa “Sayyid Sistani ameweza kupaza sauti yake kwa wairaq wote na taasisi za kitaifa na kimataifa, ukiwemo umoja wa mataifa na taasisi ya haki za binaadamu sambamba na kuwa karibu na raia wakati wote wa matatizo ya Iraq”.

Akaendelea kusema “Sayyid Sistani amekuwa akihimiza daima utoaji wa huduma bora kwa raia wa Iraq na kuidhi kwa uhuru na Amani, bila kuwepo kwa ubaguzi wa kitabaka au kimadhehebu, lilipokuja kundi la magaidi hapa Iraq na kutaka kuvunja umoja kwa kuanzisha vita ya kibaguzi baina ya wananchi, Sayyid Sistani alitoa tamko la kuhakikisha wananchi hawagawiki na kuingia kwenye vita ya wao kwa wao, tamko hilo limeifikisha Iraq katika kisiwa cha Amani”.

Akasema: “Uwepo wa Sayyid Sistani hapa Iraq unawapa raia utulivu, na maneno yake hutibu majeraha, hakika uwepo wake unafanya watu wahisi Amani”.

Muheshimiwa kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya akaendelea kusema “Anaesoma historia ya Najafu na hauza yake yenye umri wa miaka elfu moja sasa, ataona kuwa Iraq imepitia matatizo mengi, lakini Maraajii na wanachuoni walikuwa na mchango wa moja kwa moja wa kutatua matatizo hayo”, akabainisha kuwa “Sayyid Sistani amesoma vizuri historia, ndio maana alipotembelewa na Papa na kusikiliza maneno yake kuhusu historia, Papa alisema (Hakika huyu ni mtu wa Mungu)”.

Akaendelea kusema “Kilipokuja kikundi cha Alqaaida nchini Iraq mwaka 2003, kisha kikaja kikundi cha Daesh kilicho teka sehemu kubwa ya nchi, wakakaribia kuteka mji mkuu wa Baghdad pamoja na miji mitakatifu, katika mazingira yaliyojaa hofu na uwoga kwa raia wa Iraq wakati huo, alitoa fatwa ya jihadi kifaya ikawa sababu ya kuzuwia kusonga mbele kwa Daesh na kuinua ari ya wanajeshi wa Iraq, sambamba na kujitokeza mamilioni ya raia wa Iraq ambao kwa utukufu wa damu zao waliweza kuiokoa Iraq”.

Akabainisha kuwa “Zaidi ya raia milioni tatu waliitikia wito wa fatwa tukufu ya kulinda Iraq na maeneo matakatifu, kupitia vita iliyodumu miaka mitatu, walifanikiwa kukomboa ardhi yote ya Iraq kutoka kwa makundi ya magaidi, huo ulikuwa ni muda mfupi sana kuikomboa Iraq, wachambuzi wa mambo ya kivita walikadiria kuwa ili kukomboa Iraq yote itachukua miaka 10 hadi 30, lakini fatwa ya Sayyid Sistani na muitikio wa raia wa Iraq ulipelekea kupatikana kwa ushindi wa mapema”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: