Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya, imeanza kutekeleza ratiba ya vikao vya usomaji wa Qur’ani katika wilaya ya Hamza mkoani Diwaniyya.
Ratiba hiyo inasimamiwa na tawi la Maahdi ya Qur’ani katika wilaya ya Hamza chini ya Maahadi ya Qur’ani tawi la Najafu, kama sehemu ya kuendeleza maadhimisho ya kuzaliwa mbora wa wanawake Fatuma Zaharaa (a.s).
Imeanza ratiba ya kujenga uwelewa kwa kujadili (Aqika kutoka ndani ya Qur’ani), kikao hicho kimefanywa ndani ya jengo la Maahadi katika wilaya ya Hamza, Qur’ani tukufu imesomwa na msomaji wa Maahadi Murtadha Swabihi Tamimi.
Ukafuata muhadhara kutoka kwa Shekhe Hunaini Al-Aaridhwi, ameongea kuhusu historia ya Bibi Zaharaa (a.s) na nafasi yake katika uislamu, sambamba na kubainisha aya zinazo mtaja, akahimiza umuhimu wa kufata mwenendo wa Fatuma (a.s) hususan kwa wasichana na wakinamama ili kujilinda na tamaduni za kimagharibi zinazoingia katika jamii za waislamu.