Atabatu Abbasiyya tukufu imeanza utekelezaji wa programu ya kukarabati misikiti na miswala iliyopo kwenye vyuo vikuu vya Iraq.
Kiongozi wa idara ya mahusiano na vyuo vikuu katika kitengo cha mahusiano cha Atabatu Abbasiyya Sayyid Maahir Khalidi amesema “Uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya umeanza kutekeleza mradi wa kukarabati misikiti na miswala iliyopo ndani ya vyuo vikuu vya Iraq kwenye mikoa tofauti”.
Akaongeza kuwa “Programu hiyo inahusisha kufanya uchambuzi wa mahitaji ya kila msikiti, ikiwa ni pamoja na (mazulia, maktaba na turba), kwa ajili ya kuweka mazingira mazuri ya kuswali na kufanya ibada zingine”.
Akaendelea kusema “Tumeunda kamati maalum inayojumuisha wanafunzi wa vyuo husika na watumishi wa idara yetu, kwa ajili ya shughuli za ukarabati, sambamba na kusambaza vipeperushi vya hadithi za Ahlulbait (a.s) zinazohimiza kutafuta elimu”.