Shurika la Nurul-Kafeel limeonyesha bidhaa zake za chakula zinazopatikana kwenye soko la ndani.

Shirika la Nurul-Kafeel linalotoa bidhaa za chakula katika Atabatu Abbasiyya linashiriki kwenye maonyesho ya kimataifa ya 47 jijini Baghdad kwa kuonyesha bidhaa za chakula zilizopo kwenye soko la ndani.

Maonyesho hayo yameratibiwa na wizara ya biashara na shirika la maonyenho na huduma za kibiashara chini ya kauli mbiu isemayo (Iraq inaendelea), jumla ya nchi (20) zinashiriki na zaidi ya mashirika (800) ya viwanda, kilimo, biashara na utalii yanashiriki, kuanzia tarehe (10 – 19) Januari 2024m.

Kiongozi wa kitengo cha matangazo na uboreshaji Muhandisi Muhammad Atwaar amesema “Ushiriki wetu kwenye maonyesho haya, unatupa nafasi ya kuonyesha bidhaa za chakula zinazotolewa na shirika la Nurul-Kafeel zilizopo sokoni, miongoni mwa bidhaa hizo ni nyama nyekundu na nyeupe, aina zote za maziwa, bidhaa kavu na aina tofauti za vyakula”.

Akaongeza kuwa “Kushiriki kwetu maonyesho ya kimataifa Baghdad awamu ya (47) kunatoa nafasi ya kumtambulisha mwananchi bidhaa za chakula zinazotolewa na shirika letu kwa bei nafuu”.

Ushiriki wa Atabatu Abbasiyya tukufu kwenye maonyesho ya kimataifa yanayofanyika jijini Baghdad awamu ya (47), umewakilishwa na shirika la teknolojia ya viwanda na kilimo cha kisasa Khairul-Juud, shirika la Nurul-Kafeel, Shirika la Alkafeel, kitengo cha miradi ya kihandisi na kituo cha matangazo na masoko Alkafeel.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: