Maonyesho hayo yameratibiwa na wizara ya biashara na shirika la maonyenho na huduma za kibiashara chini ya kauli mbiu isemayo (Iraq inaendelea), jumla ya nchi (20) zinashiriki na Zaidi ya mashirika (800) ya viwanda, kilimo, biashara na utalii yanashiriki, kuanzia tarehe (10 – 19) Januari 2024m.
Kiongozi wa idara ya mauzo Sayyid Yaasir Aamir amesema “Hakika kushiriki kwetu kwenye maonyesha haya, ni mafanikio makubwa ya idara ya viwanda na ujenzi, kwani ni sehemu nzuri ya kuonyesha kazi zetu”.
Akaongeza kuwa “Awamu hii tumekuja na baadhi ya vitu ambavyo hatukuwa navyo katika awamu iliyopita, kama vile kiwanda cha tofali na prevel pamoja na sekta ya vioo”.
Akaendelea kusema “Lengo la kushiriki kwenye maonyesho ni kushajihisha matumizi ya bidhaa zinazotengenezwa hapa nchini)”.
Ushiriki wa Atabatu Abbasiyya tukufu kwenye maonyesho ya kimataifa yanayofanyika jijini Baghdad awamu ya (47), umewakilishwa na shirika la teknolojia ya viwanda na kilimo cha kisasa Khairul-Juud, shirika la Nurul-Kafeel, Shirika la Alkafeel, kitengo cha miradi ya kihandisi na kituo cha matangazo na masoko Alkafeel.