Sayyd Swafi ametoa wito wa kutunza masomo ya Qur’ani ya Karbala na turathi zake kwa lengo la kurithisha vizazi vijavyo.

Kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Sayyid Ahmadi Swafi, ametoa wito wa kutunza masomo ya Qur’ani na turathi zake kwa lengo la kurithisha vizazi vijavyo.

Ameyasema hayo alipotembelewa na wasomaji wa Qur’ani tukufu wa mji wa Karbala.

Sayyid Swafi amewakumbusha hali ya wasomaji wa Qur’ani wa Karbala na changamoto walizopata wakati wa utawala wa kidikteta uliopita, lakini pamoja na changamoto zote walifanikiwa kutunda elimu yao hadi imetufikia.

Akafafanua kuwa, waliweza kutunza masomo ya Qur’ani ya Karbala na turathi zake, akahimiza ulazima wa kutunza turathi kwa ajili ya vizazi vijavyo.

Akabainisha kuwa, kuna umuhimu wa kila msomaji wa Karbala apate nafasi ya kusoma ndani ya Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya kwani sauti ya Ataba hizo inafika kila sehemu ya Dunia.

Msomaji Ali Kaabi akasema, Kuna wasomaji wengi wa Qur’ani katika mji wa Karbala, pia kuna mahadhi maalum na turathi yapasa kutunzwa na kubakishwa hai.

Akaongeza kuwa, Athari ya adhana ya pamoja inayosomwa na Ataba mbili takatifu za Karbala na mahadhi ya usomaji wa Karbala yana athari nzuri katika miji mingine, sambamba na mwitikio mzuri unaopatikana kwa mazuwaru na wakazi wa mji wa Karbala.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: