Mkuu wa ofisi ya kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Dokta Afdhalu Shami amehudhuria kwenye hafla hiyo, baadhi ya wajumbe wa kamati kuu, marais wa vitengo na makamo katibu mkuu wa Atabatu Husseiniyya Sayyid Alaa Aalu Dhiyaau-Dini.
Hafla imefunguliwa kwa Qur’ani tukufu iliyosomwa na Ammaari Alhilliy, kisha ukafuata ujumbe wa uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya uliowasilishwa na mjumbe wa kamati kuu Dokta Abbasi Rashidi Dida Mussawi, akasisitiza kuwa Ataba tukufu hutumia matukio ya Ahlulbait (a.s) kama mimbari na jukwaa la kufundishia misingi ya Aqida na mafundisho ya Dini katika umma wa kiislamu.
Hafla ilikuwa na vipengele vingi, kulikuwa na kipengele cha mashairi, ambacho ameshiriki Muhammad Twahir Swafi, Muhammad Aajibi na Farasi Asadi.
Aidha kulikuwa na kipengele cha qaswida, bwana Ali Dhahabi ameimba qaswida kuhusu mazazi ya Imamu Albaaqir na Alhaadi (a.s).
Hafla ikahitimishwa kwa kuwapa zawadi watu walioshinda kwenye shindano maalum kuhusu mazazi ya Imamu Muhammad Albaaqir na Ali Alhaadi (a.s) lililoendeshwa na kitengo cha habari na utamaduni siku za nyuma.