Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya inafanya vikao vya usomaji wa Qur’ani katika mtaa wa Abbasiyya ndani ya mji wa Najafu.
Kiongozi wa idara ya usomaji katika Maahadi ya Qur’ani mjini Najafu Sayyid Ahmadi Zamiliy amesema “Vikao hivi vya ufundishaji wa Qur’ani hufanywa mara nne kwa mwezi, husomwa juzuu moja la Qur’ani kwa lengo la kujenga utamaduni wa kusoma Qur’ani kwenye maeneo tofauti ya mkoa wa Najafu”.
Akaongeza kuwa “Vikao vinahusisha kufundisha mahadhi ya usomaji wa tajwidi chini ya walimu bobezi wa fani hiyo”.
Akaendelea kusema kuwa “Majmaa Inafanya vikao hivi mara nane kila mwezi ndani ya ofisi za Maahadi na vikao vinne katika wilaya ya Mashkhabu, kwa ushiriki wa wanafunzi wake waliohitimu kwenye semina za Qur’ani tukufu, vikao hivi ni sehemu ya mkakati wa kuandaa watu watakaoshiriki kwenye ratiba ya usomaji wa Qur’ani katika mwezi mtukufu wa Ramadhani”.