Skauti ya Alkafeel imegawa mauwa na halwa katika kuadhimisha mazazi ya Imamu Albaaqir na Alhaadi (a.s).

Jumuiya ya Skaut Alkafeel chini ya kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya, imegawa mauwa na halwa (pipi) katika maeneo tofauti ndani ya mji wa Karbala wakati wa kuadhimisha mazazi ya Imamu Albaaqir na Alhaadi (a.s).

Mmoja wa viongozi wa Skaut Sayyid Muhammad Abduridhwa amesema “Kutokana na maelekezo ya uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu, tumegawa mauwa na halwa (pipi) kwa mazuwaru wa mji wa Imamu Hussein na ndugu yake Mwezi wa bani Hashim (a.s) wakati tukiadhimisha mazazi ya Imamu Muhammad Albaaqir na Ali Alhaadi (a.s)”.

Akaongeza kuwa “Tumesambaza vijana wa Skaut kwenye barabara tofauti za mji wa Karbala, kwenye vituo vya ukaguzi, vituo vya afya, pembeni ya majengo ya vyoo na maeneo yenye mkusanyiko wa watu kwa ajili ya kugawa mauwa na halwa (pipi)”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: