Idara ya Dini imefanya hafla ya kuadhimisha mazazi ya Imamu Albaaqir na Alhaadi (a.s).

Idara ya Dini tawi la wanawake katika Atabatu Abbasiyya tukufu, imefanya hafla kubwa ndani ya Sardabu ya Imamu Alkaadhim (a.s).

Kiongozi wa idara ya habari na harakati Bibi Rajaa Ali amesema “Hafla imefunguliwa kwa Qur’ani tukufu, kisha ikaelezwa historia kwa ufupi ya Imamu Muhammad Albaaqir na Ali Alhaadi (a.s), sambamba na kubainisha umuhimu wa mwanaadamu kuwa na mafungamano na Mwenyezi Mungu mtukudu pamoja na Imamu wa zama zake”.

Akaongeza kuwa “Hafla imepambwa na mashairi yaliyojaza furaha kwa wahudhuriaji, mashairi yamehimiza kuwapenda Maimamu na kizazi cha Mtume (a.s), na kuhitimishwa kwa kusoma Duau-Faraji”.

Akamaliza kwa kusema: “Lengo la kufanya maadhimisho kama haya ni kueneza mafundisho ya Ahlulbait (a.s) na kuhimiza kufuata mwenendo wao na kushikamana na kizazi kitakatifu”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: