Kitengo cha mgahawa katika Atabatu Abbasiyya kimegawa zaidi ya sahani milioni moja za chakula kwa mazuwari ndani ya mwaka 2023m.
Rais wa kitengo Sayyid Aadil Hamami amesema “Katika mwaka ulioisha tumegawa jumla ya sahani za chakula (10,513,857), idadi hiyo imezidi idadi ya sahani za chakula zilizotolewa mwaka wa nyuma yake, idadi ya wanufaika wa huduma yetu imeongezeka”.
Akaongeza kuwa, sahani zilizo tolewa wakati wa ziara ya Arubaini zilifika (6,208,984), kwenye ziara ya Ashura (417742), na ziara ya mwezi kumi na tano Shabani sahani (196205), kazi ya kugawa chakula inafanyika kwaka mzima.
Akasema kuwa, kitengo kina mkakati maalum wa kuandaa chakula na kukigawa kupitia sehemu tofauti za ndani na nje ya Ataba tukufu, huandaliwa chakula cha aina tofauti.
Akabainisha kuwa, kitengo cha mgahawa kinafanya kila kiwezalo kuhudumia idadi kubwa zaidi ya mazuwaru wa ndani na nje ya Iraq, wahudumu wake hufanya kazi kubwa sana wakati wa ziara zinazohudhuriwa na mamilioni ya watu, akasema kuwa, mgahawa wa Atabatu Abbasiyya ni wakwanza kupokea mazuwaru na wamwisho kuwaaga.