Kitengo cha maarifa kimeshiriki kwenye kongamano la turathi kwa mara ya kwanza katika mji wa Basra.

Kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kupitia kituo cha turathi za Basra, kimeshiriki kwenye kongamano la turathi kwa mara ya kwanza katika mji wa Basra.

Kongamano hilo linafanywa ndani ya jengo la utamaduni katika mji wa Basra, chini ya kauli mbiu isemayo (Tende zake zimetengeneza maisha) kwa usimamizi wa serikali ya Basra na litadumu kwa muda wa siku mbili.

Katika ushiriki huo kitengo kimeonyesha machapisho yake mbalimbali, sambamba na utafiti uliofanywa na kituo kuhusu ziara ya Arubaini na mafungamano yake na watu wa Basra pamoja na urithi wa kijamii katika maombolezo ya Husseiniyya.

Taasisi mbalimbali za kitamaduni zinashiriki kwenye kongamano hilo pamoja na vikundi vinavyo jihusisha na mambo ya turathi na utamaduni.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: