Sayyid Swafi amempongeza mmoja wa wachoraji wa Atabatu Abbasiyya kwa kuwa mshindi wa kwanza katika moja ya mashindano ya kimataifa.

Kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Sayyid Ahmadi Swafi na Sayyid Liith Mussawi wamempongeza mmoja wa wachoraji wa kitengo cha habari katika Atabatu Abbasiyya tukufu kwa kuwa mshindi wa kwanza kwenye shindano la kimataifa la (Mji mkuu wa Mawakibu).

Sayyid Swafi wakati wa kikao cha utoaji wa pongezi hizo amesema kuwa, Atabatu Abbasiyya imekuwa ikisaidia kukuza vipaji vya watumishi wake na ushindi huu nikielelezo cha wazi kwa kazi nzuri inayofanywa.

Kwa ipande wa mshindi huyo amesema “Leo tumekutana na kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Sayyid Ahmadi Swafi, kufuatia ushindi tuliopata kwenye shindano la (Mji mkuu wa Mawakibu), lililokuwa na washiriki zaidi ya (255) kutoka nchi tofauti, ikiwa ni pamoja na Pakistani, Baharain, Iraq, Marekani, nao wanauzowefu mkubwa katika fani hii, picha zaidi ya (3100) zimeshindanishwa”.

Akaongeza kuwa “Ushindi huu usingepatikana kama sio msaada endelevu tunaopewa na kiongozi mkuu wa kisheria na idara ya kitengo cha habari”, akasisitiza kuwa “Huu sio ushindi wa kwanza, tumesha wahi kushinda kwenye mashindano mengine ya kimataifa pia”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: