Idara ya wahadhiri wa Husseiniyya tawi la wanawake imewapa mtihani wanafunzi wa Maahadi ya wahadhiri.

Idara ya wahadhiri wa Husseiniyya tawi la wanawake chini ya ofisi ya kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya, imetoa mtihani wa maneno na kuandika kwa wanafunzi wa Maahadi ya wahadhiri.

Kiongozi wa idara bibi Taghridi Tamimi amesema “Maahadi huweka mikakati kila mwaka kabla ya kuanza masomo, kwa kutoa mtihani wa maneno na kuandika, kila mtihani hupewa muda maalumu”.

Akaongeza kuwa “Idara ya Maahadi inatumia mbinu za kisasa katika utoaji wa mitihani, huwapa wanafunzi nafasi ya kujadiliana baina yao kupitia maswali ya kila siku, mbinu hiyo imesaidia sana kuinua kiwango cha wanafunzi na wengi wao kufanya vizuri kwenye mitihani”.

Akabainisha kuwa “Walimu wanasahihisha karatasi za mitihani na kutunga maswali ya awamu ya pili katika kila hatua, kama wakiona kuna haja”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: