idara ya maelekezo ya kidini tawi la wanawake katika Atabatu Abbasiyya tukufu, imeandaa shindano kwa wanawake wanaokuja kumzuru Abulfadhil Abbasi (a.s).
Shindano limesimamiwa na idara ya habari, nalo ni sehemu ya kuadhimisha mazazi ya Imamu Muhammad Albaaqir na Ali Alhaadi (a.s).
Shindano limehusisha maswali kuhusu Imamu Albaaqir na Alhaadi (a.s), limelenga kutoa elimu kwa mazuwaru na kupata mazingatio kutokana na historia ya Maimamu hao watakatifu.
Lengo la shindano hilo ni kuadhimisha mazazi ya Maimamu hao watukufu na kujenga uwelewa wa Dini katika jamii, jambo hilo linafaida kubwa katika kujenga fikra ya mwanamke wa kiislamu.