Kitengo cha usimamizi na ujenzi wa kihandisi katika Atabatu Abbasiyya, kumefunga taa (900) ndani ya ukumbi wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s).
Sayyid Baaqir Ali Hassan Muhandisi katika idara ya umeme amesema “Watumishi ya idara yetu wanefunga taa za mapambo ndani ya malalo takatifu ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na maeneo yanayozunguka Ataba”.
Akaongeza kuwa “Karibu taa za mapambo (900) zimefungwa ndani ya ukumbi wa hara tukufu”.
Akasema kuwa “Ufungaji wa taa hizo ni sehemu ya mapokezi ya mwezi mtukufu wa Rajabu na Shabani sambamba na kuadhimisha mazazi ya Maimamu watakatifu waliozaliwa katika miezi hiyo”.