Kitengo cha uboreshaji na maendeleo endelevu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kimeandaa semina ya Microsoft excel kwa baadhi ya watumishi wa Ataba tukufu.
Mkufunzi wa semina Sayyid Muntadhiru Katibu amesema “Kitengo kimeandaa semina ya Microsoft excel kwa baadhi ya watumishi wa vitengo vya Ataba, kwa lengo la kuwarahisishia utendaji katika kazi zao na utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku”.
Akaongeza kuwa “Semina imedumu kwa muda wa siku sita, kila siku walikuwa wanasoma kwa muda wa saa tatu ndani ya ukumbi wa Naafidhu-Albaswirah, wamefundishwa mambo mbalimbali yanayohusu Kompyuta”.