Watumishi wa Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya, wameomboleza kifo cha Imamu Ali Alhaadi (a.s) kupitia maukibu ya pamoja katika mji wa Samaraa.
Sayyid Zamaan Yusufu mmoja wa wahudumu wa Maukibu amesema “Kutokana na tukio la kuhuzunisha la kifo cha Imamu Alhaadi (a.s), watumishi wa Ataba mbili Husseiniyya na Abbasiyya wamefanya maukibu ya pamoja katika mji wa Samaraa, kwa lengo la kuomboleza na kuhudumia mazuwaru watukufu”.
Akaongeza kuwa “Maukibu imefanya matembezi ya Amani hadi kwenye malalo ya Imamu Ali Alhaadi (a.s) huku wakiimba qaswida za kuomboleza zilizo amsha hisia za huzuni na majonzi”.
Akaendelea kusema “Maukibu ilikamilisha matembezi yake kwa kufanya majlisi ya kuomboleza ndani ya ukumbi wa haram tukufu, muhadhiri ameongea kuhusu historia ya Imamu Alhaadi (a.s) huku qaswida na tenzi za kuomboleza zikipamba majlisi hiyo”.
Watumishi wa Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya hufanya maukibu maalumu katika matukio yanayohusu Ahlulbait (a.s) wakati wote wa mwaka.