Uratibu wa kikao cha usomaji wa Qur’ani katika nchi ya Madagaska.

Kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya kupitia Markazi Dirasaati Afriqiyya, kimeratibu kikao cha usomaji wa Qur’ani katika nchi ya Madagaska.

Mkuu wa Markazi Shekhe Saadi Satari Shimri amesema “Markazi Dirasaati Afriqiyya imefanya kikao cha usomaji wa Qur’ani cha kwanza katika mwaka huu wa (2024) katika nchi ya Madagaska, chini ya usimamizi wa muwakilishi wa Markazi Shekhe Abdulmaliki Salstini, kimehudhuriwa na kundi kubwa la waumini na wafuasi wa Ahlulbait (a.s)”.

Akaongeza kuwa “Kisomo cha Qur’ani ni sehemu ya ratiba ya mwezi mtukufu wa Rajabu, kutakuwa na vipengele vingi vinavyo lenga kuwakumbusha watu umuhimu wa Qur’ani tukufu”.

Markazi Dirasaati Afriqiyya inaimarisha uhusiano na makundi tofauti ya jamii katika bara la Afrika kupitia program hizi, sambamba na kuwafanya watu waendelee kuipenda Qur’ani tukufu na kuitukuza.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: