Atabatu Abbasiyya inafanya shindano la kitamaduni kuhusu mazazi ya Imamu Aljawaadi (a.s).

Uongozi mkuu wa Ayabatu Abbasiyya unafanya shindano la kitamaduni kuhusu mazazi ya Imamu Muhammad Aljawadi (a.s).

Majina ya washindi kumi wa mwanzo yatatangazwa siku ya Jumapili tarehe (21/1/2024m) saa moja jioni, kwenye jukwaa la Atabatu Abbasiyya tukufu.

Sharti la kupokea zawadi, mshindi anatakiwa awepo kwenye hafla ya kuzaliwa Imamu Aljawaadi (a.s) itakayofanywa kwenye eneo la mlango wa Kibla ya Abulfadhil Abbasi (a.s) siku ya Jumatatu (22/1/2024m) sawa na mwezi (10 Rajabu 1445h), iwapo mshindi atakuwa na udhuru wa kuhudhuria kwenye hafla hiyo, atatakiwa kufika kwenye ofisi za mali (wahasibu) ndani ya muda usiozidi siku nne toka kutangazwa kwa matokeo, akiwa na kitambulisho cha uraia au hati ya kusafiria.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: