Kitengo cha Habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya tukufu kimeandaa ziara ya Pamoja kwa wanafunzi wa Dini wenye asili ya Afrika wanaosoma Najafu, ya Kwenda kutembelea makaburi ya mashahidi wa fatwa ya jihadi kifaya ya kujilinda.
Ziara imeratibiwa na Markazi Dirasaati Afriqiyya chini ya kitengo, kwa kushirikiana na kikosi cha Imamu Ali (a.s).
Mkuu wa Markazi Shekhe Saadi Sataari Shimri amesema “Ziara hii ni sehemu ya kuangalia ushujaa wa walimu wa hauza na wanafunzi wao walioitikia wito wa Marjaa Dini mkuu wa fatwa ya jihadi kifaya kwa ajili ya kulinda taifa na maeneo matakatifu”.
Akaongeza kuwa “Wanafunzi wataangalia ushujaa wa mashahidi waliojitolea kila kitu kwa ajili ya kulinda taifa la Iraq na raia wake, Pamoja na maeneo matakatifu, ugeni wa wanafunzi hao umefanya majlisi ya kuomboleza na kusoma Qur’ani kwa ajili ya roho za mashahidi”.
Akaendelea kusema “Ziara inalenga kuangazia sifa za kimaadili, kielimu na kitawala kwa mashahidi, waliwakilisha zama muhimu katika historia ya Iraq, wajibu wetu kwao ni kuenzi historia hii tukufu”.
Mwisho wa ziara hiyo, kikosi cha Imamu Ali (a.s) kikakabidhi bendera ya jihadi kwa Markazi, aidha wanafunzi wa Dini wenye asili ya Afrika wameshukuru uongozi wa Markazi kwa kazi kubwa wanayofanya ya kuwasimamia na kuratibu ziara za Pamoja zinazo waonyesha historia ya Iraq na ushujaa wa watu wake.