Hivi karibuni kitengo cha Habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya kimechapisha kitabu cha (Dini na changamoto za kijamii) ikiwa ni muendelezo wa vitabu vya Dini.
Kitabu kimechapishwa chini ya usimamizi wa kituo cha kiislamu na tafiti za kimkakati chini ya kitengo, kimeandikwa na jopo la watafiti na kuhaririwa na Sayyid Muhammad Hussein Kiyani.
Kitabu kimeandika vitu tofauti, miongoni mwake ni, Mantiki, milango ya kijamii, Qur’ani, hadithi, Akhlaq, mambo ya kijamii, njia za kupambana na ufisadi wa kiidara kwa kufuata misingi ya uislamu, kupambana na ufakiri kwa kutumia mbinu za kiislamu, mikakati ya maimamu katika kupambana na changamoto za kijamii, elimu ya maradhi ya nafsi na tabia mbaya.
Kitabu kimepangwa kwa anuani, miongoni mwa anuani hizo ni mabadiliko ya jamii katika mtazamo wa Qur’ani, kiwango cha Maisha na kuharibika kwa jamii, njia za kudhibiti mmomonyoko wa maadili katika jamii, athari ya itikadi za Dini katika kupunguza mmomonyoko wa maadili kwenye jamii, nafasi ya familia katika kupambana na uharibifu wa jamii na utamaduni, Pamoja na mambo ya kifiqhi na kiuchumi.